Manispaa yaingia hasara ya Sh400 milioni
Morogoro. Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imepata hasara ya Sh400 milioni baada ya kusitisha kutoza ushuru kwa wafanyabiashara wa Soko Kuu kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu sasa.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga alisema manispaa hiyo ilipata mkopo wa Sh7.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa soko hilo unaotarajiwa kugharimu Sh16 bilioni.
Alisema kuchelewa kuanza kwa ukarabati na ujenzi wa soko hilo lililojengwa 1953, kumesababishwa na ukosefu wa fedha.
Hata hivyo, alisema tayari mchakato wa kuomba mkopo kutoka Benki ya CRDB wa fedha hizo kwa awamu, umekamilika na kupatiwa Sh7.5 bilioni. Kihanga alisema ujenzi huo utakamilika kwa kipindi cha mwaka mmoja utaanza muda wowote mwezi huu.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wafanyabiashara kuunga mkono jitihada hizo kwa kuondoka kwa hiyari sokoni hapo.
Alisema baada ya ujenzi huo kukamiliki, watatoa kipaumbele kwa wafanyabiashara waliokuwapo awali sokoni hapo.
Mapema mwaka 2014, manispaa hiyo ilitoa notisi kwa wafanyabiashara wote sokoni hapo ya kuwataka kutotoza ushuru kwa madai kuwa wangehamishwa na kupelekwa kwenye eneo jingine kupisha ujenzi huo wa soko hilo jipya na la kisasa.
Mmoja wa wafanyabiashara wa sokoni hapo, Ismail Rashid alisema mazingira ya soko hilo kuanzia majengo mpaka miundombinu mingine imechakaa.
Alisema mvua zikinyesha, hukumbwa na mafuriko ya majitaka kwa sababu lilijengwa wakati manispaa ikiwa na idadi ndogo ya wafanyabiashara na watumiaji wengine.
Source:Mwananchi
Manispaa yaingia hasara ya Sh400 milioni
Reviewed by Zero Degree
on
1/12/2016 01:53:00 PM
Rating: