Loading...

Maofisa watatu Halmashauri Geita kizimbani kwa wizi wa milioni 31.6.


Geita. Aliyekuwa Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Victor Swai; Mlipa fedha, Sundi Makonda na Ofisa Mipango, James Masolo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Geita na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakikabiliwa na makosa mawili ya uhujumu uchumi, likiwamo la wizi wa zaidi ya Sh31.6 milioni.



Mwanasheria wa Takukuru wa mkoa huo, Osborn Pais akisaidiana na Augustino Mtaki, alidai mbele ya Hakimu Safina Simfukwe alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 21, 2010.

Watuhumiwa hao walikana mashtaka na kuachiwa baada ya kutimiza masharti kwa kila mmoja kulipa nusu ya fedha wanazotuhumiwa kuiba au kuweka dhamana ya mali yenye thamani hiyo na wadhamini wawili wenye mali au nusu ya fedha hizo.

Hakimu Simfukwe aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 11, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.



Source: Mwananchi
Maofisa watatu Halmashauri Geita kizimbani kwa wizi wa milioni 31.6. Maofisa watatu Halmashauri Geita kizimbani kwa wizi wa milioni 31.6. Reviewed by Zero Degree on 1/12/2016 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.