Loading...

Moto Wazua Taharuki Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani [ Tazama Picha hapa ]



Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nchi wakiwa katika wamesimama nje ya jengo hilo baada ya kutokea hitilafu ya cheche za umeme katika gholofa ya nne.




Wafanyakazi ambao walipata mshtuko wa ghafla wakiwa nje ya jengo hilo.


Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi wanaofanya kazi zao katika jengo hilo la wizara ya mambo ya ndani wakitoka nje baada ya hitilafu hiyo.Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SSP, Advera Senzo Bulimba,akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la wizara ya mambo ya ndani ya nchi baada ya kutokea cheche za moto katika jengo hilo katika gholofa ya nne na kusema kuwa baada ya tukio hilo uongozi wa wizara hiyo waliwapigia simu jeshi la zimamoto ambao walifika muda sahihi na kuangalia chanzo cha moto huo na akaongeza kwa kusema kuwa hakuna mfanyakazi yoyote katika jengo hilo aliyedhurika kutokana na cheche hizo za moto zilizoonekana katika cyling board.Gari la kikosi cha zimamoto likiwa katika eneo la tukio tayari kuzima moto endapo ungedhuru jengo hilo.

Wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa nje ya jengo, pembeni ni gari la zimamoto.

Mapema leo asubuhi, jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam lilinusurika kuwaka moto baada ya kutokea cheche za umeme ndani ya jengo hilo na kuzua taharuki kwa watu waliokuwemo ndani ya jengo hilo kabla ya Kikosi cha Zimamoto kufanikiwa kuudhiti moto huo.


Source: GPL

Comment & Share this!!

Moto Wazua Taharuki Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani [ Tazama Picha hapa ] Moto Wazua Taharuki Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani [ Tazama Picha hapa ] Reviewed by Zero Degree on 1/06/2016 08:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.