Loading...

Nauli yakwamisha mabasi yaendayo kasi kuanza kazi.


Daladala zikipakia abiria kwenye Kituo cha Kimara, Dar es Salaam jana baada ya kushindikana kuanza kazi kwa mabasi yaendayo haraka. 


Dar es Salaam. Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaka mradi wa mabasi yaendayo haraka kuanza juzi limekwama kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa kukusanya maoni ya kiwango cha nauli.

Majaliwa alitoa agizo hilo Desemba 19, mwaka jana alipokuwa akikagua barabara za mabasi hayo, agizo ambalo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Tamisemi, Selemani Jaffo alisema limekuwa likiwanyima usingizi.

Kampuni inayoendesha mradi huo, Uda-RT ilipendekeza viwango vya nauli vya Sh700, Sh1,200 na Sh1,400 ambavyo vilikataliwa na wadau na Serikali kwa maelezo kuwa zitawaumiza wananchi.

Akizungumza jana, msemaji wa Uda-RT, Sabri Mabruk alisema mradi huo umeshindwa kuanza kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa viwango vya nauli ambao unaratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti na Huduma za Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).

“Mchakato wa kukusanya maoni ya nauli haujakamilika, ndiyo maana unaona mradi haujaanza, lakini tunatarajia hadi wiki ijayo huenda ukawa tayari,” alisema.

Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema ukusanyaji wa maoni juu ya nauli unaendelea hadi kesho. Hatuwezi kutangaza nauli wakati ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi bado unaendelea, kanuni ya tozo za nauli ya mwaka 2009 inasema maoni yakusanywe ndani ya siku 14 na siku bado hazijaisha,” alisema Mziray.



Source: Mwananchi
Nauli yakwamisha mabasi yaendayo kasi kuanza kazi. Nauli yakwamisha mabasi yaendayo kasi kuanza kazi. Reviewed by Zero Degree on 1/12/2016 02:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.