Loading...

Ukawa watuma barua kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachewene wakitaka wapewe sababu za kuahirishwa uchaguzi wa Meya Dar.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachewene.      

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Ukawa, kimemuandikia barua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachewene ikimtaka aeleze kwa kina sababu za kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam. Wiki iliyopita, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ilitangaza kuahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 23 bila kueleza sababu zaidi ya kuwataka wakazi kusubiri tarehe nyingine.

Siku iliyofuata, Simbachawene alitangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika Februari 8 na kusema uliahirishwa kutokana na mfumo wa upatikanaji wa Baraza la Jiji linaloundwa na madiwani kutokana Kinondoni, Ilala na Temeke akisema zamani katika chama kimoja hakukuwa na shida kubwa kuhusu upatikanaji wake. 

Hata hivyo, hakutoa ufafanuzi zaidi. Katibu wa Chadema, Kanda ya Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema jana kuwa Ukawa wakiwa wadau, bado hawajapewa taarifa rasmi za kuahirishwa kwa uchaguzi huo, zaidi ya kusoma na kuona kupitia vyombo vya habari. 

“Tungependa kupata ufafanuzi wa kina juu ya kauli hii na kama kuwa na chama kimoja au vingi kunabadilisha chochote hasa kwa wajumbe wanaopaswa kupiga kura,” alisema Kilewo.



Source: Mwananchi
Ukawa watuma barua kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachewene wakitaka wapewe sababu za kuahirishwa uchaguzi wa Meya Dar. Ukawa watuma barua kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachewene wakitaka wapewe sababu za kuahirishwa uchaguzi wa Meya Dar. Reviewed by Zero Degree on 1/28/2016 12:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.