Loading...

Zikiwa zimebaki siku 21 kufanyika uchaguzi Mkuu nchini Uganda, picha za Raisi Museveni zachanwa huku kampeni za wagombea uraisi zikiendelea.


Mgombea urais wa Uganda, Amama Mbabazi akikata keki kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwenye Wilaya ya Lwengo jana.



Hoima. Zikiwa zimebaki siku 21 kufanyika uchaguzi Mkuu nchini Uganda wagombea wa urais wanaendelea kufanya kampeni zao huku kukiwa na matukio mbalimbali nchini humo.

Jana, polisi walimkamata mfuasi wa Chama cha FDC, kwa madai ya kumuona akichana picha ya mgombea urais Rais Yoweri Museveni.

Tukio hilo lilitokea kwenye Wilaya ya Hoima na picha hizo zilibandikwa kwenye ukuta wa duka kubwa la Kyarushesha na mfuasi huyo wa FDC alionekana akizichana na kuzitupa chini.

Msemaji wa polisi wilayani hapo Lydia Tumushabe, alisema mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ambrose Tumukwase, anashikiliwa na polisi kwa kosa hilo.

“Alionekana akizichana picha za Museveni na kuweka za mgombea wa chama chake Dk Kiiza Besigye, hivyo tunamshikilia kwa mahojiano zaidi,’’ alisema Tumukwase.

“Kwa kawaida kuchana picha za mgombea ni kosa na sisi tunachokitaka ni kusimamia amani ya nchi hivyo tunaendelea kumhoji kwanza,” alisema. 


Mgombea urais kupitia Chama cha ‘Forum for Democratic Change’ Kizza Besigye amesema hakuna sababu kwa chama tawala cha NRM kusherehekea siku ya ukombozi kwa sababu familia kadhaa za Waganda ambao ndugu zao walimwaga damu hawajanufaika kwa lolote.

Amama Mbabazi alisema, wananchi wa Uganda wanataka mabadiliko ili maisha yao mazuri. Alisema miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na walimu kupewa maishara mikubwa pamoja na madaktari ambao ni sekta muhimu kwa wananchi.

 “Hakuna nchi ambayo inaendelea bila kuwajali walimu na madaktari kwani inashangaza leo tunasikia walimu na madaktari wamegoma kwa kudai mishahara hii ni aibu kwa nchi’’alisema.


Source: Mwananchi
Zikiwa zimebaki siku 21 kufanyika uchaguzi Mkuu nchini Uganda, picha za Raisi Museveni zachanwa huku kampeni za wagombea uraisi zikiendelea. Zikiwa zimebaki siku 21 kufanyika uchaguzi Mkuu nchini Uganda, picha za Raisi Museveni zachanwa huku kampeni za wagombea uraisi zikiendelea. Reviewed by Zero Degree on 1/28/2016 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.