Loading...

Hii hapa siri ya kuifunga Simba SC, aliyoianika Amisi Tambwe.


Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ameanika sababu za kuifunga Simba mara mbili mfululizo katika msimu huu kuwa ni uchezeaji wao wa kiungwana pamoja na ubora wa timu yake.



Tambwe aliyesajiliwa na Yanga akitokea Simba msimu uliopita, alifunga bao wakati timu hizo zilipokutana kwenye mzunguko wa kwanza Septemba mwaka jana, kabla ya kufunga bao lingine katika mechi ya Jumamosi. 


Tambwe alisema amefanikiwa kuifunga Simba kutokana na aina ya uchezaji wao wa kutoka kamia sambamba na ubora wa timu yake. Alisema ni rahisi kuifunga Simba kwani inacheza soka linalofanana na Yanga, huku pia mabeki wake wengi kutocheza soka la kukamia kama ambavyo wachezaji wa timu nyingine wanavyocheza wanapokutana na Yanga.

“Simba inacheza mpira mzuri na wala hawakamii kama ambavyo wachezaji wa timu nyingine hutuchezea pale unapokutana nao, hivyo ni rahisi kucheza nao. Pia sisi tuna wachezaji wazuri ambao wana uwezo wa kupigania ushindi,” alisema Tambwe.

Tambwe akiwa amefunga mabao 15, katika Ligi Kuu akiwa nyuma Hamis Kiiza mwenye mabao 16, alisema mkakati wake ni kuibuka mfungaji bora.

“Ninachokifikiria sasa ni kufunga katika mechi zetu zote zilizosalia, najua nitakuwa na upinzani, lakini nitapambana kuhakikisha natimiza malengo yangu.

“Niliazimia kufanya hivyo katika mchezo na Simba, nilipiga magoti kumuomba Mwenyezi Mungu na kweli nimefanikiwa, lakini sasa nahitaji kufanya hivyo katika kila mchezo nikipewa nafasi ya kucheza,” alisema Tambwe.



ZeroDegree.
Hii hapa siri ya kuifunga Simba SC, aliyoianika Amisi Tambwe. Hii hapa siri ya kuifunga Simba SC, aliyoianika Amisi Tambwe. Reviewed by Zero Degree on 2/22/2016 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.