Polisi Kanda Maalumu Dar imeanza kukamata bodaboda zinazovunja sheria na kusababisha ajali barabarani.
Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeanza kuwakamata madereva wa bodaboda wanaovunja sheria na kusababisha ajali barabarani.
Kamanda Simon Sirro amesema operesheni hiyo inafanyika katika wilaya zote za jiji kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya uhalifu na ajali zinazosababishwa na pikipiki.
Kutokana na operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Wilaya ya Ilala, Omary Kombo ameitupia lawama polisi kwa kuendesha kamata kamata bila kuwashirikisha.
Kombo amelalamika mwenzao mmoja alipoteza maisha wakati akijaribu kuwakimbia askari waliokuwa kwenye msako huo.
“Kuna wakati tunakamatwa hata pasipo na hatia na kibaya zaidi tunatozwa faini kubwa ya Sh90,000 kwa kosa moja, ingekuwa vizuri kama viongozi tungeshirikishwa katika jambo hili,” amesema.
Amesema jeshi hilo limekuwa likitumia nguvu kuwakamata na wakati mwingine kuwabambikia makosa.
Dereva wa bodaboda, Hamis Hussein amesema polisi huwakamata kwa madai kuwa wanawatafuta wahalifu ambao madereva hao wanawajua.
“Sisi siyo wahalifu tunafanya kazi tupate kipato kinachotuwezesha kujikimu maisha yetu,” amesema.
ZeroDegree.
Polisi Kanda Maalumu Dar imeanza kukamata bodaboda zinazovunja sheria na kusababisha ajali barabarani.
Reviewed by Zero Degree
on
2/06/2016 07:08:00 PM
Rating: