Loading...

Hiace yateleza kwenye kivuko, na kisha kutumbukia baharini Jijini Dar.


Jeshi la Zimamoto linaendelea kuutafuta mwili wa mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari aina ya Hiace ambalo limetumbukia bahari ya Hindi leo alfajiri mara baada ya kuteleza kutoka kwenye kivuko kilichokuwa kinaelekea upande wa Kigamboni. 

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi hilo, Briton Monyo, ajali hiyo imetokea majira ya saa 10 alfajiri na hadi sasa wameweza kuupata mwili wa dereva wa gari hilo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 29-30.

Monyo anasema gari hilo litakuwa limetitia chini kwa eneo ambalo tukio limetokea lina kina kirefu cha maji, tope jingi na vumbi na huku jeshi likiwa halina vifaa kama darubini ya majini.

Hata hivyo, ndugu wa mwanamke anayetafutwa wanasema jana walitoka Mbeya kwenye msiba wa ndugu yao na gari walilopanda la magazeti liliwaacha eneo Feri saa 10 alfajiri wakati huo kivuko kilikuwa kimefika ndipo walipoingia na kukutana na Hiace na kukubaliana na dereva kuwafikisha makwao mara baada ya kuvuka ng’ambo ya pili.

Hata hivyo, mwanamke huyo alikuwa amechoka na kuingia ndani ya Hiace kabla huku ndugu wengine tisa wakakaa sehemu ya abiria ya kivuko.

“Lakini kabla panton halijaanza kuondoka tulishangaa Hiace ikiserereka na kutumbukia kinachowashangaza zaidi,” mmoja wa ndugu hao alisema.

Source: Mwananchi



ZeroDegree.
Hiace yateleza kwenye kivuko, na kisha kutumbukia baharini Jijini Dar. Hiace yateleza kwenye kivuko, na kisha kutumbukia baharini Jijini Dar. Reviewed by Zero Degree on 4/20/2016 01:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.