Loading...

Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, imewatia mbaroni raia tisa wa China kwa kuingia nchini kinyume na sheria.


Idara ya Uhamiaji imewanasa raia tisa wa China kwa kufanya kazi wilayani Kyerwa bila kuwa na vibali halali. 

Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, Abdalah Towo, raia hao waliajiriwa na kampuni ya George Joseph Kizenga Company Limited ya jijini Dar es salaam.

Waliokamatwa ni Changyuan Jia,Yongzhi Liu, Baoyin Qian, Bing Sunchen na Yuan Tangbao. Wengine ni Yuan Piangjing, Yuan Chi, Piangliang Yuan na Liu Huabao.

Akitoa taarifa ya utendaji kwa kipindi cha miezi mitatu (Januari hadi Machi), Towo alisema kuwa jumla ya raia 675 kutoka mataifa mbalimbali walikamatwa na wengine kufikishwa mahakamani.

Nchi za Rwanda na Burundi zinaongoza kwa kuwa na raia wengi wa kigeni waliokamatwa mkoani Kagera ambao huingia kupitia vituo vya Omurusagamba na Kabanga kutokana na machafuko ya kisiasa. Katika kipindi hicho, jumla ya Wanyarwanda 137 na Warundi 353 wamekwishakamatwa.




ZeroDegree.
Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, imewatia mbaroni raia tisa wa China kwa kuingia nchini kinyume na sheria. Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, imewatia mbaroni raia tisa wa China kwa kuingia nchini kinyume na sheria. Reviewed by Zero Degree on 4/20/2016 01:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.