Loading...

Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini.


Dodoma. Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amesema mwisho wa kutumika kwa mifuko ya plastiki nchini itakuwa Januari Mosi mwaka 2017.

Katika swali lake la nyongeza Mbunge wa Njombe Mjini, (CCM), Edward Mwalongo alitaka kujua ni lini ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) itakaa na wadau wa Mazingira.

Akijibu swali hilo Makamba alisema sasa wanaendelea na mazungumzo kwa kushirikisha wadau na wakati wa bajeti ya wizara yake ana imani kuwa watakuwa wamefika mwisho.

Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua iwapo serikali haioni umefikia wakati wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri hiyo Luhaga Mpina, alisema serikali inaona umuhimu wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo ambapo katika utekelezaji wa hilo walipitia upya kanuni za kuzuzia uzalishaji, uagizaji, uuzaji, ununuzi na matumizi ya mifuko hiyo ya mwaka 2006 ambayo ilipiga marufuku mifuko chini ya mikroni.

Hata hivyo alisema kanuni hizo zinazoonekana kuwa changamoto katika utekelezaji wake.

Pia alisema, serikali iliandaa kanuni mpya za matumizi ya mifuko ya za mwaka 2015, kanuni hizo zilifuta kanuni ya 2006 na kuweka viwango vipya vya mifuko na vifungashio vya plastiki kuwa na unene usiopungua mikroni 50 ambayo inauwezo wa kuoza kirahisi kwenye mazingira ukilinganisha na ile ya mikroni 30.

Mpina alifafanua kuwa, pamoja na kuongeza unene wa mifuko ya plastiki, kanuni hiyo inapiga marufuku uanzishwaji wa viwanda vipya vya kutengeneza mifuko ya plastiki ambayo ipo chini ya viwango vilivyobainishwa na kanuni.

“Katika kuimarisha uwekezaji katika sekta ya mazingira na kuhamasisha uwekezaji katika teknolojia rafiki ya mazingira, serikali inaandaa kauni na taratibu za nyenzo za kiuchumi zitakazotoa ruzuku,” alisema.





ZeroDegree.
Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini. Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini. Reviewed by Zero Degree on 4/20/2016 02:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.