Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm ataka kuweka rekodi mpya ya kuchukua ubingwa Afrika.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van Pluijm
Dar es Salaam. Baada ya kuipa Yanga ubingwa wa pili mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Hans Pluijm amesema sasa malengo yake ni kuweka rekodi mpya katika mashindano ya Afrika.
Akizungumza baada ya kushuhudia timu yake ikitoka sare ya mabao 2-2 na Ndanda kabla ya kukabidhiwa kombe juzi, Pluijm alisema bado anaona nafasi nyingine ya mafanikio makubwa zaidi kwa timu kwa kufika mbali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuanzia timu hiyo kutinga hatua ya makundi.
Mara ya mwisho Yanga kutinga hatua ya makundi katika mashindano ya Afrika ilikuwa 1998 katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hata hivyo ilimaliza ikiwa ya mwisho katika kundi lake.
Jumatano watashuka uwanjani kuivaa Sagrada Esperanca ya Angola wakihitaji sare yoyote au ushindi wa ugenini ili kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikisalia na mechi moja, kocha Pluijm amegundua kikosi chake bado kina nguvu ya kufanya vyema kutokana na wachezaji wake kuonyesha kuwa wana uwezo na hawajachoka ni jambo ambalo anataka kulitumia kuhakikisha wanafika mbali katika mashindano hayo ikiwa ni timu pekee ya ukanda wa Afrika Mashariki iliyosalia katika mashindano ngazi ya klabu Afrika.
“Tunastahili kupata sifa na mafanikio ya namna hii, tumekuwa na msimu mgumu na bora ambao utulivu wetu na viwango vyetu vimetufanya sasa kutembea kifua mbele, tunaweza kupata mafanikio zaidi katika Afrika msimu huu,” alisema Pluijm.
“Angalia timu yangu, tuko mwisho mwa msimu, lakini bado timu inaonekana kuhitaji kucheza zaidi, akili yetu sasa ni kuhakikisha tunafika mbali katika mashindano ya Afrika, hii ni nafasi muhimu kwetu kuipa sura mpya klabu hii,” alisema Pluijm, ambaye mkataba wake na mabingwa hao unamalizika wiki tatu zijazo.
“Kwa sasa siwezi kuzungumzia suala la mkataba wangu hadi pale nitakapofuzu katika hatua ya makundi, nitakuwa katika nafasi nzuri ya kujadili suala hilo.”
Wakati Pluijm akisema hivyo, nahodha wake beki mkongwe Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amemuomba kocha huyo kutoruhusu usajili mkubwa kufanyika katika kipindi hiki kwa kuwa bado kikosi chao kina nguvu.
Cannavaro alisema mabadiliko makubwa yatakayofanyika katika usajili yanaweza kuirudisha nyuma timu hiyo kwa kuanza upya msimu ujao, jambo ambalo linaweza kuwapa shida, lakini akamuachia Pluijm nafasi ya kufanya uamuzi.
“Najua suala la kusajili ni uamuzi wa kocha, lakini kwangu nikiwa kama nahodha naona bado Yanga tuna timu bora na yenye ushindani, lakini kuna nafasi za kuzifanyia maboresho.”

Nahodha Cannavaro atoa neno

ZeroDegree.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm ataka kuweka rekodi mpya ya kuchukua ubingwa Afrika.
Reviewed by Zero Degree
on
5/16/2016 11:44:00 AM
Rating: