Loading...

Mabaki ya ndege ya Egypt Air yapatikana


Timu ya waokoaji kutoka Misri, Ufaransa, Ugiriki na Uingereza inaendelea na msako mkali katika bahari ya Mediteranian kusaka ndege iliyoanguka jana wakati ikielekea Cairo kutoka Paris huku kukiibuka taarifa zinazotofautiana kuhusu kuoneka kwa mabaki hayo.

Awali, taarifa zilisema kuwa Wizara ya Usafiri wa Anga nchini Misri imepokea barua rasmi kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje nchini humo inayothibitisha kupatikana kwa mabaki ya ndege iliotoweka ya MS 804 karibu na kisiwa cha Karpathos.

Katika kwenda sambamba na taarifa hiyo kampuni hiyo ilituma salamu za rambirambi kwa familia za abiria na wafanyikazi waliokuwa wakiabiri ndege hiyo. Tayari familia za abiria hao pamoja na wafanyikazi wameelezewa kuhusu tukio hilo jipya.

Baadaye Serikali ya Misri ilitoa taarifa kukanusha taarifa za kuonekana kwa mabaki hayo huku ikisisitiza kuendelea na msako. Taarifa hiyo haikueleza zaidi mbali ya kusisitiza kuwa “ Serikali inapenda kufuta taarifa yake ya awali kuhusu kuonekana kwa mabaki hayo,”.

Kwa sasa kundi la wachunguzi wa Misri wakishirikiana na wenzao wa Ugiriki, Ufaransa na wale wa Uingereza wanaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo iliyokuwa na watu 66, wengi wao wakiwa ni raia wa Misri na Ufaransa.

Ndege hiyo ilikuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.

Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmojammoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Chad na Ureno. Awalia Rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa amesema kuwa ndege hiyo ilianguka.

Kumekuwa na hisia kuwa huenda ndege hiyo ilitunguliwa na mabaki na siyo kwamba ilikumbwa na hitilafu ya kiufundi.

Jeshi la Misri na shirika la safari za ndege nchini humo zimesema kuwa mabaki ya ndege ya EgyptAir iliotoweka yamepatikana katika bahari ya Mediterranean.

Msemaji wa jeshi la Misri alisema kuwa mabaki na abiria wa ndege hiyo walipatikana kilomita 290 kutoka mji wa Alexandria.

Katika taarifa yake, Rais Abdel Fattah al-Sisi alisikitishwa na ajali hiyo.

Kampuni ya ndege ya EgyptAir pia ilithibitisha kupatikana kwa mabaki hayo katika mtandao wake wa Twitter.



Mataifa ya Ugiriki,Misri,Ufaransa na Jeshi la Uingereza yamekuwa yakishiriki katika oparesheni ya kuisaka ndege hiyo karibu na kisiwa cha Karpathos.

Ugiriki inasema kuwa rada yake imekuwa ikionyesha kwamba ndege hiyo iligeuka kwa ghafla mara mbili na kuanguka kutoka futi 25,000 na kuingia katika maji.

ZeroDegree.
Mabaki ya ndege ya Egypt Air yapatikana Mabaki ya ndege ya Egypt Air yapatikana Reviewed by Zero Degree on 5/20/2016 06:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.