Loading...

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta atinga Ligi ya Europa.


Genk, Ubelgiji. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kufuzu kucheza Ligi ya Europa baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5-1 na kushinda kwa jumla ya mabao 5-3.

Samatta, ambaye katika mchezo wa kwanza walionyukwa 2-0 alianzia benchi, jana aliaminiwa kuanza mchezo huo na kocha wake Peter Maes, akicheza pamoja na Nikos Karelis katika safu ya bora ya ushambuliaji.

Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao moja na kutegeneza mengine mawili yaliyofungwa na Karelis ambaye alifunga magoli matatu katika mchezo huo, na Sandy Walsh akifunga bao moja kabla ya Sporting Charleroi kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Jeremy Perbet.

Genk, ikicheza kwenye wake wa nyumbani wa Cristal Arena ilianza mchezo kwa kasi na dakika 16, ilipata penalti baada ya Samatta kuangushwa kwenye eneo la hatari na kipa Nicolas Penneteau, ambaye alipewa kadi nyekundu. Karelis alifunga penalti hiyo kwa Genk.

Samata aliwainua mashabiki wa Genk kwa kupachika bao la pili akiungamisha mpira uliotemwa na kipa wa Sporting, Penneteau katika dakika 27, kabla ya Sporting Charleroi kupata bao dakika 40 lililofungwa na Jeremy Perbet na kuifanya timu hizo kwenda mapumziko ikiongoza kwa mabao 2-1.

Genk ilianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Sandy Walsh.

Ushirikiano mzuri baina ya Samatta na Karelis ulisaidia kupatika kwa bao la nne wakati Mtanzania huyo alipokimbia na mpira na kuwa katika nafasi mbili za kutoa pasi kwa Bailey au Karelis. 

Samagol alimpa Bailey aliyeusukumia mpira wavuni. Karelis alihitimisha kwa kufunga bao la tano.




ZeroDegree.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta atinga Ligi ya Europa. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta atinga Ligi ya Europa. Reviewed by Zero Degree on 5/30/2016 04:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.