Mwanafunzi Arusha, amekamatwa na polisi akidaiwa kutoa taarifa za uchochezi kwa njia ya Mtandao.
Arusha. Mwanafunzi wa mwaka wa tatu, Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI), Mkazi wa Arusha, amekamatwa na polisi akidaiwa kutoa taarifa za uchochezi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema Mmbando alituma ujumbe huo kupitia mtandao wake Facebook na kuandika maneno yanayodaiwa ya uchochezi.
Maneno hayo yanayodaiwa kuwa ya lieleza kuwa: “Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje, halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti.”
Ujumbe mwingine unaodaiwa kusambazwa na mtuhumiwa huyo aliousambaza kwa kutumia mtandao wake wa Facebook ni:
“Dk Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kushtuka, namuomba Mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisiasa hasa watawala na si wananchi wa kawaida.”
Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbe, mwanafunzi huyo alikamatwa Mei 17 saa 3:00 asubuhi na kwamba, baada ya upekezi wa simu yake ilibainika alituma ujumbe huo Mei 7.
“Baada ya uchunguzi kukamilika, atapelekwa mahakamani,” alisema Mkumbo.
Alitoa rai kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuitumia vizuri kwa kuzingatia Sheria ya Mitandao, hivyo alitoa onyo kwa wengine wanaotumia mitandao hiyo nje ya nchi kuwa iwapo watakiuka sheria ya mitandao hawataonewa haya.
Hivi karibuni, mtoto wa aliyekuwa Mwanasiasa nchini, Chacha Wangwe, Bob Wangwe aliwekwa rumande kwa kosa la kuchapisha habari za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kuwa ni koloni lake.
Awali, Bob alikiri kutenda kosa hilo, lakini baada ya kupandishwa kizimbani Mei 17 alikana shtaka hilo.
ZeroDegree.
Mwanafunzi Arusha, amekamatwa na polisi akidaiwa kutoa taarifa za uchochezi kwa njia ya Mtandao.
Reviewed by Zero Degree
on
5/21/2016 02:23:00 PM
Rating: