Tume ya Haki za Binadamu yalaani kitendo cha udhalilishaji wa mwanamke kilichotokea Dakawa [ Mkoani MOROGORO ].
Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga.
Dar es Salaam. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inalaani vikali ubakaji na udhalilishaji wa mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa) mnamo Aprili 27 mwaka huu huko Dakawa, Wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro.
Wabakaji hao walimrekodi mwanamke huyo na kuisambaza video ya tukio hilo katika mitandao ya kijamii kitendo ambacho ni cha udhalilishaji wa mwanamke huyo, uhuru na haki ya faragha, na utu wake pia.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Tume hiyo, Bahame Tom Nyanduga, alilipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua za haraka ilizozichukua za kuwakamata waliohusika, kuwafikisha mahakamani kujibu mashtaka, ili sheria ichukue mkondo wake.
“Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inatambua kwamba binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa na kwamba kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake, kama ilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na mikataba na matamko mbalimbali ya kimataifa kuhusu ya haki za wanawake” alisema
Kadhalika taarifa hiyo ilieleza kuwa Tume inawakumbusha wananchi wote, wajibu wa kila mtu wa kulinda na kuheshimu haki za binadamu, zikiwamo haki za wanawake, wajibu ambao ni msingi mkubwa wa kuhakikisha taifa linajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.
ZeroDegree.
Tume ya Haki za Binadamu yalaani kitendo cha udhalilishaji wa mwanamke kilichotokea Dakawa [ Mkoani MOROGORO ].
Reviewed by Zero Degree
on
5/21/2016 10:17:00 AM
Rating: