Wavaa MILEGEZO sasa kutandikwa viboko hadharani.
Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, kuadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.
Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika sambamba na kupiga marufuku uvaaji suruali kwa wanawake pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria na kufikia makubaliako kuwa zoezi hilo litafanyika hadharani huku adhabu hiyo pia ikiwahusisha wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.
ZeroDegree.
Wavaa MILEGEZO sasa kutandikwa viboko hadharani.
Reviewed by Zero Degree
on
5/16/2016 11:14:00 AM
Rating: