Breaking News: Kocha Stephen Keshi aaga dunia.
Wakati Dunia inasubiri kumpumzisha Mohammad Ali kesho, Maumivu mengine yatakayodumu mioyoni mwa wapenzi wa Soka ni kuondokewa kwa kipenzi chao Stephen Keshi aliyewahi kuwa nahodha na baadae kocha wa Timu ya Taifa ya soka ya Nigeria.
Nyakati zote akiwa nahodha mwaka 1994,Super Eagles ilitwaa ubingwa kwa kuilaza Zambia bao 2-1,mjini Tunis na kisha mwaka 2013,mjini Johannesburg kwenye uwanja wa Soccer City Super Eagles kwa mara nyingine ikiwa chini ya ukufunzi wake ikailaza Burkinafaso bao 1-0.
Rekodi hiyo ilimfanya Keshi kuwa Binadamu wa pili Barani Afrika kutwaa Ubingwa wa Mataifa Barani Afrika akiwa mchezaji tena nahodha na baadae akiwa kocha. Rekodi kama hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mohamed El ghohari wa Misri
Steven Atakumbukwa kwa mchango wake katika soka la Nigeria ambapo alikuwa kwenye kikosi kilichotinga hatua ya 16,bora mwaka 1994,kwenye fainali za soka kombe la Dunia nchini Marekani pamoja na kusumbuliwa na maumivu ya goti yaliyohitimisha soka lake mapema.

Super Eagles ikiwa na majina ya kutosha mwaka huo akina Peter Rufai, Austin Eguavoen, Benedict Iroha, Uche Okechukwu,C hidi Nwanu, Sunday Oliseh, bila kumsahau kiungo mahiri Austin Jay Jay Okocha, Rashid Yekini, Daniel Amokachi, Emmanuel Amunike na George Finidi walizitandika Bulgaria na Greece na kuweza kutinga raundi ya pili kabla ya safari yao kuhitimishwa na Italia iliyokuwa na akina Roberto Baggio ambaye alizima ndogo za Nigeria dakika za majeruhi baada ya Emmanuel Amunike kutangulia mapema nyavuni mwa Wataliano.
ZeroDegree.
Breaking News: Kocha Stephen Keshi aaga dunia.
Reviewed by Zero Degree
on
6/09/2016 05:27:00 PM
Rating: