Loading...

Goodluck Ole Medeye [ CHADEMA ] atimkia chama cha UDP.


Goodluck Ole Medeye.

Aliyekuwa Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw. Goodluck Ole Medeye amehamia rasmi Chama cha UDP kinachoongozwa na Bw. John Cheyo na kukabidhiwa kadi ya uanachama leo.

Ole Medeye ni mbunge wa zamani wa Jimbo la Arumeru Magharibi ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika awamu ya nne, lakini pia aliteuliwa na vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.


Goodluck Ole Medeye akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wakati alipojiunga akitokea CCM.

Medceye ametangaza uamuzi huo wakati akiongea na wanahabari ambapo amesema UDP inasimamia haki na demokrasia na yeye anataka demokrasia ya kweli na jukwaa la haki katika kuleta haki na maendeleo kwa Watanzania.

Source: GPL
ZeroDegree.
Goodluck Ole Medeye [ CHADEMA ] atimkia chama cha UDP. Goodluck Ole Medeye [ CHADEMA ] atimkia chama cha UDP. Reviewed by Zero Degree on 6/12/2016 06:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.