Loading...

Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.


Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemtangaza Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya Dkt. Charles Kitwanga aliyefutwa kazi hivi karibuni.

Nafasi ya Mwigulu katika Wizara ya Kilimo na Uvuvi imechukuliwa na Injinia Dkt. Charles Tizeba, Mbunge wa Buchosa mkoani Mwanza ambaye katika uongozi wa awamu ya nne, aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu alikuwa waziri wa Kilimo na Mifugo.



Waziri Mpya wa Kilimo na Mifugo, Dkt. Charles Tizeba.


Uteuzi wa Mwigulu umepongezwa na wengi katika mitandao ya kijamii, baadhi yao wakidai ni mchapakazi atakayeweza kuimudu wizara hiyo mpya yenye changamoto nyingi, hasa uhalifu wa kutumia silaha, biashara ya unga na rushwa.

Akiwa katika wizara ya Kilimo na Uvuvi, Mwigulu alianza kazi yake kwa kasi kubwa, akisimamia kwa karibu migogoro ya ardhi inayowahusu wakulima na wafugaji, hasa wa eneo la Mvomero mkoani Morogoro, ambako alifanikisha ujenzi wa uzio unaotenganisha maeneo ya jamii hizo mbili.

Charles Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alifutwa kazi na Dk. Magufuli Mei 20 mwaka huu, miezi mitano tu tokea alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika Baraza la kwanza la Mawaziri wa serikali ya awamu ya tano, kwa madai ya kutumia kilevi wakati wa saa za kazi.

Mawaziri walioteuliwa leo wataapishwa na rais Magufuli keshokutwa, Jumatatu June 13, 201, Ikulu Jijini Dar es Salaam, saa 3:00 asubuhi.




ZeroDegree.

Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Reviewed by Zero Degree on 6/12/2016 06:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.