Loading...

Papa Fransis kuwashusha madaraka maaskofu watakaoshindwa kushughulikia makasisi wanaonyanyasa watoto kingono.



Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Fransis ametangaza kuwa maaskofu wa kanisa hilo watakaoshindwa kushughulikia makasisi waliokumbwa na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto wadogo wanaweza kuondolewa katika madaraka yao.


Sheria mpya ya Vatican iliyotolewa na Baba Mtakatifu Jumamosi inaonekana kuwa ni majibu yaliyotafutwa muda mrefu na wanaharakati wa kikatoliki nchini Marekani ambao walipinga walichokiona ni kushindwa kuchukuliwa hatua dhidi ya makasisi waliotenda uovu huo.

Agizo la Baba Mtakatifu limeweka wazi kwamba hata wale maaskofu ambao hawashutumiwi kuwanyanyasa kingono watoto wanaweza kuondolewa kwenye nafasi zao kama wataonekana wameshindwa kuchukua hatua na kulinda waumini wao kutokana na manyanyaso ya mapadri.

Maaskofu tayari wanauwezekano mkubwa wa kuwajibishwa au kupoteza nafasi zao za kazi kama sababu kuu zitathibitishwa. Waathiriwa wa manyanyaso hayo nchini marekani na kwingineko duniani kwa muda mrefu wamelalamika kwamba baadhi ya maaskofu wanapuuzia au kuficha vitendo vya unyanyasaji ndani ya kanisa.

Source: VOA Swahili
ZeroDegree.
Papa Fransis kuwashusha madaraka maaskofu watakaoshindwa kushughulikia makasisi wanaonyanyasa watoto kingono. Papa Fransis kuwashusha madaraka maaskofu watakaoshindwa kushughulikia makasisi wanaonyanyasa watoto kingono. Reviewed by Zero Degree on 6/05/2016 11:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.