Loading...

Tume ya Taifa ya Uchaguzi [ NEC ] Waikosoa Ripoti ya WAANGALIZI WA UCHAGUZI toka Umoja wa Ulaya [ EU ].


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kuhusu ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, iliyowasilishwa na Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU).

NEC imesisitiza kwamba ripoti hiyo imebainisha mapungufu ambayo hayapo kwenye sheria na taratibu, zinazoiongoza tume hiyo.


Miongoni mwa mapungufu waliyoyatoa waangalizi hao ni Suala la Uchaguzi wa Zanzibar, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na haki ya wagombea binafsi kugombea nafasi katika uchaguzi wowote wa Tanzania Bara na Zanzibar, mgawanyo wa majimbo na uwazi wa kuhesabu kura.


Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima.

Akitoa ufafanuzi huo, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, waliwapa nafasi hiyo waangalizi wa ndani na nje kuangalia uchaguzi wa Tanzania Bara , kama unaenda kulingana na Katiba, sheria na taratibu za uchaguzi huo.

Alisema kuwa katika ripoti hiyo, waangalizi hao wamezungumzia uchaguzi wa Zanzibar, ambao NEC hawahusiki nao na kwamba wamefanya makosa, kwa kuwa wao walikuwa waangalizi wa uchaguzi wa Tanzania Bara na sio Zanzibar.

‘’Waangalizi wowote wa uchaguzi wanapoomba kibali kuangalia uchaguzi, wanatakiwa kufuata taratibu kwa kutambua kwamba kuna NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Sisi tulitoa kibali kwa waangalizi hawa kuangalia uchaguzi wetu na sio wa Zanzibar,’’ alisema.

Aliongeza kuwa, ‘’hawakupaswa kuingiza katika ripoti yao masuala ya uchaguzi wa Zanzibar ulivyokuwa, badala yake wangeeleza kama NEC hatukufuata sheria na taratibu kwenye uchaguzi huu wa Tanzania Bara.”


Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi [ NEC ] Waikosoa Ripoti ya WAANGALIZI WA UCHAGUZI toka Umoja wa Ulaya [ EU ]. Tume ya Taifa ya Uchaguzi [ NEC ] Waikosoa Ripoti ya WAANGALIZI WA UCHAGUZI toka Umoja wa Ulaya [ EU ]. Reviewed by Zero Degree on 6/05/2016 12:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.