Loading...

Ajuza abakwa na kuuawa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo.

CHRISTINA Mnyira (89) mkazi wa Patandi wilayani Arumeru mkoani Arusha amekutwa amekufa baada ya kubakwa na kunyongwa shingo.

Mnyira alikutwa amekufa Julai 21 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo alisema kijana mmoja ametiwa mbaroni na mwingine anasakwa.

Alisema baada ya bibi huyo kufanyiwa unyama huo mwili wake ulitupwa katika msitu wa Chuo cha Mifugo Tengeru na wasamaria wema walitoa taarifa polisi.

ZeroDegree.
Ajuza abakwa na kuuawa Ajuza abakwa na kuuawa Reviewed by Zero Degree on 7/28/2016 10:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.