Loading...

Antonio Conte amalizana na Diego Costa.

Hatma ya mshambualiaji wa Chelsea, Diego Costa imekuwa haijulikani kutokana na kocha mpya wa timu hiyo, Antonio Conte kuwa hajazungumzia jambo hilo na kufanya tetesi za Costa kurejea Atletico Madrid kuongezeka.

Wakati wakiwa katika kujiandaa na msimu wa 2016/2017, kocha Conte amemaliza maneno kuhusu habari hizo kwa kuwatoa hofu mashabiki wa Chelsea na wa soka kwa ujumla kuwa Costa ataendelea kuitumikia klabu hiyo na ana furaha kuwepo Chelsea,

“Diego Costa ni mchezaji wetu, ni mchezaji mwenye uwezo wa kipekee na ana umuhimu mkubwa,” alisema Conte na kuongeza kuwa “Ana furaha kuwa hapa na anafanya mazoezi kwa kujituma”

Aidha Conte alimzungumzia beki wa timu hiyo, Kurt Zouma ambaye alipata majeruhi mwezi Februari mwaka huu na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, “Tunajua Zouma anafanya mazoezi ili kurejea hali yake ya awali, lakini anahitaji muda, ni muhimu iwe hivyo na hatumpeleki haraka katika hilo”


ZeroDegree.
Antonio Conte amalizana na Diego Costa. Antonio Conte amalizana na Diego Costa. Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 09:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.