Loading...

Majina ya marehemu yatumika kuomba mikopo toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu [ HESLB ].

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema wakati Bodi ya Mikopo
ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ikiendelea kufanya uchumbuzi kuhusu wanafunzi wanaostahili kupokea mikopo wamebaini kuwa kuna wanafunzi wengine wameshafariki lakini majina yao yamekuwa yakitumika kuomba mikopo.

Waziri Ndalichako aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatma ya wanafunzi 7,805 waliorudishwa nyumbani mwezi Mei mwaka huu baada ya walimu waliokuwa wakiwafundisha kufanya mgomo.

Alisema pamoja na kukuta majina ya wengine ambao wameshafariki yakitumika kuomba mikopo lakini pia kuna majina ya wanafunzi wengine wameshafukuzwa vyuo lakini nao bado majina yao yanaonekana kuomba mkopo.

“Pesa za mkopo bado hatujazitoa sababu tunataka kujiridhisha kama wanafunzi ambao tunawapa pesa wanastahili kupata mkopo, katika kipindi hiki ambacho tumeshakagua baadhi ya vyuo tumegundua kuwepo na wanafunzi ambao wameshafariki na bado majina yao yanatumika kuomba mikopo,

“Ukiacha hilo vipo vyuo viwili na majina vilikuwa vikileta lakini tumechunguza na kuona kuna wanafunzi wengine wameombewa mikopo lakini walishafukuzwa vyuo tena wengine tangu mwaka 2013,” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha aliongeza kuwa msimamo wa serikali upo palepale kuwa utaanza kutoa mikopo mpaka pale utakapojiridhisha kuwa wanafunzi wote ambao wanapatiwa mikopo wanakadhi vigezo na kinyume na hapo mikopo kwa wanafunzi wote wataizuia.



ZeroDegree.
Majina ya marehemu yatumika kuomba mikopo toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu [ HESLB ]. Majina ya marehemu yatumika kuomba mikopo toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu [ HESLB ]. Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 10:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.