Loading...

Waandaaji wa filamu zilizokamatwa waanzaa kujisalisalimisha Bodi ya Filamu

Baadhi ya waaandaaji wa Filamu nchini waanza kujisalimisha Bodi ya Filamu Tanzania baada ya Filamu zao kukamatwa zikiwa sokoni wakati hazijafanyiwa uhakiki na Bodi hiyo.

Haya yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo alipokuwa akifanya mahojiano na mmoja wa waandaaji wa Filamu nchini aliyekutwa na kadhia hiyo Bw. Akim Igembe kutoka Kampuni ya Akim Master Film baada ya Filamu yake ijulikanayo kwa jina la “Mapenzi Uchizi” bango lake lilikutwa sokoni likiwa na alama ya Uhakiki kutoka Bodi ya Filamu wakati ilikuwa bado haijahakikiwa na Bodi hiyo.

Operesheni ya kukamata Filamu zilizoingizwa sokoni kinyume cha sheria ambayo ilimshirikisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ki ukweli imekuwa ya mafanikio sana maana sasa wameanza kujileta wenyewe,

“Wakati tunapitia fomu ya Uhakiki wa Filamu hii tulibaini kuwa ni moja kati ya kazi tulizozikamata kutokana na kuwa na alama ya uhakiki bila kupitia kwetu, tena ikiwa na daraja 18 wakati katika daraja hali la filamu hiyo inapaswa kuwa ni daraja 16,” alisema Fissoo.

Awali akitoa utetezi wake mbele ya watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, muandaaji wa Filamu ya Mapenzi Uchizi Bw. Akim Igembe kutoka Akim Master Film amesema pamoja na kuwa ndiye mmiliki wa Filamu hiyo, ahusiki moja kwa moja na mabango yaliyokutwa sokoni ya kiitangaza filamu hiyo kwani bado ndiyo alikuwa anafuatilia kibali kutoka Bodi ya Filamu.

Nakuongeza kuwa ata yeye mwenyewe anashangaa kuona mabango yanayoitangaza Filamu hiyo ili hali alikuwa bado haijafanyiwa uhakiki na Bodi ya Filamu na kwanza ndiyo alikuwa anafuatilia kibali.

Ata hivyo alieleza kuwa Master ya Filamu hiyo aliiuza kwa mfanyabiara mmoja kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyemtaja kwa jina la Baraka Sunzu uende ndeye aliyehusikana na udanganyifu huo.

Akihitimisha mahojiano na mtuhumiwa huyo Katibu huyo amesema ofisi yake imeamua kuchukua uamuzi wa kuzuia Kibali cha Filamu hiyo hadi hapo atakapopatikana mfanyabiashara Raia wa Congo, Baraka Sunzu anayedaiwa kuuziwa kazi hiyo na kudurufu atakapo patikana kutoa maelezo ya wapi alipata nembo hiyo ambayo imetumika kinyume cha sheria na watakapojiridhisha hatua stahiki zitachukuliwa.


ZeroDegree.
Waandaaji wa filamu zilizokamatwa waanzaa kujisalisalimisha Bodi ya Filamu Waandaaji wa filamu zilizokamatwa waanzaa kujisalisalimisha Bodi ya Filamu Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 09:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.