Loading...

Azam mguu sawa kuvaana na Yanga ngao ya hisani.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd.

TIMU ya Azam FC inatarajiwa kurudi leo kutoka Zanzibar kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kumenyana na Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 17 mwaka huu.

Azam ilikuwa Zanzibar kwa kambi ya wiki moja. Timu hiyo ilicheza mechi mbili za kirafiki na itaendelea na mazoezi yake ya kawaida kwenye uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd alisema wanarudi kuendelea na maandalizi yao ikiwa na wachezaji wapya ambapo kocha atatoa majibu ya nani atabaki kwa ajili ya kupewa mkataba.

“Tunashukuru tunaendelea vizuri, tutarudi kuendelea na maandalizi yetu huko kuungana na wachezaji wengine waliosajiliwa, tuna imani tayari kocha wetu Zeben Hernandez anajua ni wachezaji gani atakuwa nao msimu ujao,”alisema.

Msemaji huyo alisema tayari mchezaji wa Medeama ya Ghana, Enock Atta Agyei, amewasili jana kuungana na kikosi hicho kwa maandalizi ya msimu mpya.

Mchezaji huyo amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili, Pia, alisema Azam tayari imemalizana na Simba ili wachezaji wake Mwadini Ali na Ame Ally kujiunga na klabu hiyo ya Msimbazi kwa mkopo.

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Azam mguu sawa kuvaana na Yanga ngao ya hisani. Azam mguu sawa kuvaana na Yanga ngao ya hisani. Reviewed by Zero Degree on 7/31/2016 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.