Loading...

CUF yamjia juu IGP Mangu.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Salum Bimani.

SIKU moja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, kusema kuwa jeshi hilo linakusududia kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa madai ya kuchochea vurugu Zanzibar, chama hicho kimesema kitendo cha kukamatwa kiongozi wao kitasababisha mpasuko mkubwa wa kisiasa visiwani humo.

Akizungumza na Nipashe mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Salum Bimani, alisema kauli ya mkuu huyo wa jeshi la polisi dhidi ya Maalim Seif imeleta mshtuko mkubwa kwa wafuasi na viongozi wa chama hicho na endapo atakamatwa na kuwekwa ndani kutapelekea mpasuko mkubwa wa kisiasa kwa kile alichosema ndiye kinara katika kuhubiri amani na kuwatuliza wafuasi wake kulinda amani.

Alisema AGP Mangu hana ushahidi wowote kuhusu madai hayo dhidi ya Maalim Seif bali ni utashi na tuhuma zinazotolewa na Chama Cha Mapinduzi dhidi ya kiongozi wao wafuasi wa chama hicho.

“Tunamshangaa sana AGP Mangu kutoa kauli hiyo kamwe Maalim hajapata kuogopa kukamatwa na jeshi la polisi kisha kushtakiwa kwa tuhuma za uchochezi.”

“Kama jeshi hilo linataka kumkamata Maalim Seif na kumuweka ndani haitakuwa mara ya kwanza, mwaka 1989 lilimkamata na kumuweka ndani kwa muda wa miaka mitatu,” alisema Bimani.

Alisema kipindi hichoo Maalim Seif alikuwa waziri kiongozi mstaafu wa serikali ya Zanzibar na aliwekwa ndani kwa tuhuma hizohizo alizozieleza AGP Mangu, lakini baadae alitolewa bila ya kuwa na hatia yoyote.

Alisema Maalim Seif hivi sasa yupo katika ziara zake nje ya nchi kwa ajili ya kudai demokrasia ambayo alidai imeporwa Oktoba 25, mwaka jana na kwamba viongozi wa CUF wanatarajia kukutana na kutoa tamko rasmi kuhusiana na kauli ya AGP.


Source: IPPMedia.com
Zerodegree.
CUF yamjia juu IGP Mangu. CUF yamjia juu IGP Mangu. Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.