Loading...

Kesi ya Halima Mdee na wenzake yapigwa kalenda tena.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi inayowakabili wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Halima Mdee (Kawe) na Saed Kubenea (Ubungo), dhidi ya tuhuma ya kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS), Theresia Mbando, hadi Agosti 29, mwaka huu.

Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi, baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hata hivyo, wakati kesi hiyo inaahirishwa jana, Mdee hakuwapo mahakamani.

Mbali na Mdee na Kubenea, washtakiwa wengine ni, Mwita Waitara, Ukonga, Diwani wa kata ya Kimara, Ephrein Kinyafu na mfanyabiashara, Rafii Juma, Diwani wa kata ya Kimanga, Manase Njema.

Washtakiwa wote wanadaiwa kuwa, Februari 27, mwaka huu katika ukumbi wa Karimjee wilayani Ilala, walmjeruhi Mbando na kumsababishia majeraha.

Awali, washtakiwa waliposomewa mashitaka yao kwa nyakati tofauti, walikana.

ZeroDegree.
Kesi ya Halima Mdee na wenzake yapigwa kalenda tena. Kesi ya Halima Mdee na wenzake yapigwa kalenda tena. Reviewed by Zero Degree on 7/28/2016 10:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.