Loading...

Kiwango cha chini cha mshahara ni Sh.100,000/= kwa mwezi.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Antony Mavunde.

Dodoma. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Antony Mavunde amesema kiwango cha chini cha mshahara bado ni Sh100,000 kwa mwezi.

Mavunde alitoa taarifa hiyo bungeni jana akisema viwango hivyo hupitiwa kila baada ya miaka mitatu. 

Alikuwa akijibu swali la mbunge wa Konde Khatibu (CUF), Said Haji aliyetaka kujua ni mfumo upi na viwango gani vilivyowekwa kisheria wanavyotakiwa kulipwa wafanyakazi wa viwanda na kampuni binafsi.

Naibu Waziri alisema mfumo unaotumika katika kupanga viwango vya chini vya mishahara vinasimamiwa na taratibu zilizoainishwa katika Sheria Namba 7 ya Taasisi za Kazi ya Mwaka 2014.

Alisema sheria imetoa pia madaraka kwa waziri mwenye dhamana ya kazi kuunda bodi moja ya kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi.

Mavunde alisema bodi hiyo inaundwa na wajumbe 17 ikiwa na wawakilishi wa wafanyakazi, waajiri na Serikali yenye jukumu la kupanga kima cha chini cha mshahara katika sekta hiyo.



Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Kiwango cha chini cha mshahara ni Sh.100,000/= kwa mwezi. Kiwango cha chini cha mshahara ni Sh.100,000/= kwa mwezi. Reviewed by Zero Degree on 7/01/2016 11:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.