Mfanyabiashara Mohamed Dewji [ Mo ], atangaza raha Simba.
Mohamed Dewji anataka kutumia bajeti ya Sh bilioni 5.5 kwa msimu kwa ajili ya Simba SC, ili kuwapiku wapinzani wao, Azam FC na Yanga.
Dewji alisema jana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, kwenye ofisi zake zilizopo jengo la Golden Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam.
Alisema atayafanya hayo iwapo Simba watakubali kumuuzia asilimia 51 ya hisa kwa Sh bilioni 20.
Alisema akiuziwa hisa hizo kuwa mmiliki wa Simba, atawawezesha wanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo kupewa hisa bure, ambazo wataamua wenyewe kuuza, au kununua hisa zaidi. Ofa hiyo imekuja wakati Simba kesho inatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka jijini Dar es Salaam.
“Shabaha yangu ni kuitoa klabu kwenye bajeti ya Sh bilioni 1.2 hadi bilioni 5.5, mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, lazima tusajili vizuri, tuajiri kocha mzuri. Ukitenga Sh bilioni 4 kwa mwaka, tayari umewazidi wapinzani Azam na Yanga.”
Na kuhusu bilioni 1.5 inayobaki, Mo Dewji alisema Simba inatimiza miaka 80 tangu ianzishwe mwaka 1936, lakini haina hata uwanja wa mazoezi. “Mimi kama mpenzi wa Simba inaniuma, wenzetu (Azam) wameanza juzi, lakini wana uwanja. Mimi nitaweka Sh bilioni 1.5 kila mwaka ili kukamilisha ujenzi wa uwanja ndani ya miaka mitatu, ambao utakuwa wa kisasa utakaotupa fursa ya kuanzisha na miradi ya soka ya vijana.”
Amesema lengo lake ni kuifanya Simba itwae ubingwa wa Afrika kwa kushindana na timu kama TP Mazembe zinazotumia bajeti ya Sh bilioni 20 kwa mwaka.
Mo Dewji ni mpenzi na mwanachama wa Simba SC, ambaye kati ya 1999 na 2005 alikuwa mdhamini mkuu wa klabu na akazishawishi pia Simba Cement na NBC kuwekeza katika klabu hiyo hadi ikafuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003 ikimtoa bingwa mtetezi Zamalek ya Misri.
Mo pia amewahi kuwa mdhamini wa Singida United na mmiliki wa African Lyon kwa muda, kabla ya kuiuza kwa mfanyabishara Rahim ‘Zamunda’ Kangenzi.

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Mfanyabiashara Mohamed Dewji [ Mo ], atangaza raha Simba.
Reviewed by Zero Degree
on
7/30/2016 09:24:00 AM
Rating: