Loading...

Profesa Rutasitara ameteuliwa na Rais kuwa Makamu MwenyeKiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga [ TCAA ].

RAIS John Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu jana Dar es Salaam, Profesa Rutasitara anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Nyamajeje Weggoro ambaye muda wake umemalizika.

Uteuzi huu umeanza Julai 16, mwaka huu. Ikulu ilieleza kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya mwaka 1977, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Mwenyekiti akitoka Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti hutoka Tanzania Zanzibar na kinyume chake.

Aidha, Rais John Magufuli amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Kedmon Mnubi kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Taarifa ya Ikulu ilieleza kuwa SACP Mnubi pamoja na makamishna wengine 59 ambao Rais Magufuli amewapandisha vyeo kuanzia juzi, watakula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Ikulu Jijini Dar es salaam saa 3:00 asubuhi.


ZeroDegree.
Profesa Rutasitara ameteuliwa na Rais kuwa Makamu MwenyeKiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga [ TCAA ]. Profesa Rutasitara ameteuliwa na Rais kuwa Makamu MwenyeKiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga [ TCAA ]. Reviewed by Zero Degree on 7/18/2016 12:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.