Loading...

Tetemeko la ardhi laathiri zaidi nyumba 60 Mkoani Dodoma.

Chamwino. Zaidi ya nyumba 60 katika Kijiji cha Kwahemu, Kata ya Haneti wilayani Chamwino zimeathiriwa na tetemeko la ardhi wiki hii katika nyumba hizo kuna zilizoanguka na nyingine kupata nyufa.

Tetemeko hilo lililotokea eneo la Haneti lilikuwa na ukubwa wa 5.1 kwa kipimo cha Richter, wakati la mwaka 2007 lililotokea Oldonyo Lengai ukubwa wake ulikuwa ni 5.9.

Tetemeko hilo lililotokea saa 12.01 asubuhi na kudumu kwa sekunde 30, kitovu chake kilikuwa ni kilomita 11 Mashariki mwa Mji wa Haneti.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Soiti, Simon Hangala alisema jana kuwa asilimia kubwa ya nyumba kwenye kijiji chake zimeathiriwa na tetemeko hilo, lakini 60 ndizo zilizoathirika zaidi.

“Nilihisi udongo unaniangukia kwa kweli tuliogopa sana kwa sababu lilikuwa ni tetemeko kubwa kuwahi kutokea katika eneo hili,” amesema Hangala.

Mkazi wa kijiji hicho, Hawa Hamis amesema siku hiyo ilimlazimu kukimbia akiwa amebeba watoto wake huku akiwa hajui mahali pa kwenda.

“Tulikuwa tumelala nikashangaa baada ya kutokea tetemeko hilo mume wangu akainuka na kukimbilia nje. Ilibidi nibebe watoto wangu hawa mapacha na kukimbia nje ya nyumba,” amesema.

Tetemeko hilo limesababisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuogopa kuingia ndani ya nyumba zao wakihofia litarejea tena.

Awali, Ofisa Mwandamizi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Gabrel Mbogoni alisema kiwango hicho cha tetemeko ni kikubwa na kinaweza kuleta madhara katika majengo na miundombinu.


ZeroDegree.
Tetemeko la ardhi laathiri zaidi nyumba 60 Mkoani Dodoma. Tetemeko la ardhi laathiri zaidi nyumba 60 Mkoani Dodoma. Reviewed by Zero Degree on 7/16/2016 10:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.