Loading...

Treni kuanzia kituo kikuu cha Stesheni hadi Pugu kuanza kazi rasmi Agosti 1, 2016.

KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL), imeanzisha treni ya pili ya usafiri jijini Dar es Salaam maarufu kama 'treni ya Mwakyembe' itakayoanza kazi keshokutwa (Tar 1, Agosti mwaka huu), ambayo itafanya safari zake kuanzia kituo kikuu cha Stesheni hadi Pugu.

Treni hiyo itakuwa ikipita katika vituo 10 ikiwamo Kamata, Mwisho wa Lami, Vingunguti, Gongo la Mboto, FFU Mombasa, Banana pamoja na Karakata.

Aidha kuongezwa kwa usafiri huo, kumesababisha mabadiliko ya ratiba ya treni kutoka Dar es Salaam kwenda bara, kuanzia Agosti 2 mwaka huu kwani itaanza safari zake kuanzia saa 9 alasiri badala ya saa 11 jioni kama ilivyokuwa awali.

Ofisa Uhusiano wa TRL, Masanja Kadogosa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kwamba treni hiyo ya pili imeongezwa ili kuboresha huduma ya usafiri kwa wakazi jijini.

"Ujio wa treni ya pili (treni ya Mwakyembe) itakayoanza Agosti Mosi mwaka huu umeleta mabadiliko ya treni iendayo bara, kutoka hapa Dar kwenda Kigoma au Mwanza, itakuwa inaanza safari jijini Dar es Salaam saa 9 alasiri tofauti na awali ilikuwa ikitoka saa 11 jioni," alisema Kadogosa.

Alisema treni hiyo ya Mwakyembe, itasafiri umbali wa kilomita 20 kwa dakika 32, kutoka Stesheni hadi Pugu na itatoza nauli ya Sh. 600 kwa kila abiria na kwamba kwa sasa itaanza na mabehewa saba na iwapo mahitaji yataongezeka mabehewa yataongezwa na kufikia 10.

ZeroDegree.
Treni kuanzia kituo kikuu cha Stesheni hadi Pugu kuanza kazi rasmi Agosti 1, 2016. Treni kuanzia kituo kikuu cha Stesheni hadi Pugu kuanza kazi rasmi Agosti 1, 2016. Reviewed by Zero Degree on 7/30/2016 09:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.