Loading...

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania [ TCU ] kuanza kudahili wanafunzi wa kujiunga vyuo vikuu kesho.

Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31.


Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao.

Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu.

Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.


ZeroDegree.
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania [ TCU ] kuanza kudahili wanafunzi wa kujiunga vyuo vikuu kesho. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania [ TCU ] kuanza kudahili wanafunzi wa kujiunga vyuo vikuu kesho. Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.