Loading...

Ukawa waichomolea CCM.

“Sasa huu ni unafiki hatuwezi kuuvumilia. Tumeshindwa kulileta Taifa pamoja. Kwa nini tukafanye unafiki wa aina hiyo wakati chama hicho tawala kimeshindwa kutuleta pamoja?” James Mbaia 

Licha ya kupata mwaliko, vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimesema havitahudhuria Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Julai 23, mjini Dodoma.

Vyama hivyo, ambavyo pamoja na vyama vingine vimealikwa kuhudhuria mkutano huo, vimesema utu wao hauwezi kuongozwa na mihemko.

Msimamo huo ni mwendelezo wa Ukawa kususia shughuli za viongozi na wabunge wa CCM tangu walipoanza kwa kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.


Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Ukawa waichomolea CCM. Ukawa waichomolea CCM. Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.