Vikao vya Kamati za Bunge sasa kufanyika Dodoma badala ya Dar.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu.
VIKAO vya Kamati za Bunge, ambavyo vilikuwa vikifanyika katika kumbi mbalimbali jijini Dar es Salaam, kuanzia sasa vitafanyika mjini Dodoma, taarifa ya Spika wa Bunge Job Ndugai ilieleza hayo jana.
Taarifa iliyosainiwa na Ndugai katika waraka wa spika namba 6/2016 kuhusu vikao hivyo, ilisema kufuatia serikali pamoja na mawaziri kutakiwa kuhamia mjini Dodoma, kamati hizo zitakuwa zikifanyika Dodoma tofauti na ilivyokuwa awali.
Taarifa ilisema vikao vya kamati hizo vitafanyika mjini humo, vitaanza Agosti 22 hadi Septemba mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa nne wa bunge, linalotarajiwa kuanza Septemba 6 mwaka huu.
Taarifa ilieleza kuwa waratibu wa shughuli za vikao hivyo, watoa huduma za utawala na watumishi watatakiwa nao kuhamia Dodoma kwa ajili ya uratibu wa shughuli hizo.
"Huko mbele tutatathmini iwapo mfumo wa sasa wa mikutano ya bunge kutanguliwa na vikao vya kamati za kudumu za bunge kuwa ndio unaotufaa, baadae tutaangalia mfumo bora zaidi wa kuunganisha vikao vya kamati pamoja na bunge, kutokana na bunge, serikali kuwa katika mji mmoja, kama ilivyo kwa nchi nyingine," ilisema taarifa hiyo na kuongeza... "Kwa mujibu wa kanuni ya bunge 117 (4) ya kanuni za kudumu za bunge, toleo la mwaka 2016, inayosema 'Mikutano ya kawaida ya kamati za bunge za kudumu itafanyika Dodoma, Dar es Salaam au Zanzibar, vikao hivyo vitafanyika mjini Dodoma kuanzia sasa," ilisema.

ZeroDegree.
Vikao vya Kamati za Bunge sasa kufanyika Dodoma badala ya Dar.
Reviewed by Zero Degree
on
7/31/2016 08:40:00 AM
Rating: