Loading...

Wadau wa soka walilia uwanja wa kisasa Dodoma.

WADAU wa michezo wameitaka Serikali kujenga uwanja wa michezo wa kimataifa mkoani Dodoma kama ule wa Taifa jijini Dar es Salaam kutokana na mpango wa kuhamishia makao makuu Dodoma.

Hayo yalisemwa mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipokutana na viongozi mbalimbali kujadiliana mpango mkakati ya Serikali kuhamia Dodoma.

Wakati wa kikao kicho kikiendelea mdau wa michezo mkoani Dodoma, Ramadhan Muzazi, alimwandikia ujumbe mwongozaji wa shughuli hiyo (MC), Peter Mavunde akimtaka amsomee Waziri Mkuu ujumbe wa wadau wa michezo wa mkoa wa Dodoma.

Mara baada ya Mavunde kupokea ujumbe huo aliusoma, ambapo wadau wa michezo mkoani Dodoma wanaomba uwanja wa kisasa kama ilivyo kwa Jiji la Dar es Salaam.

“Kuna ujumbe nimepewa hapa naomba niusome,unasema hivi,mmejadili mambo mengi lakini hatujasikia suala la michezo. Je, sisi wana Dodoma kutokana na makao makuu kuhamia hapa, vipi tutapata uwanja wa kisasa kama ule wa Dar es salaam,”alisema Mavunde.

Baada ya ujumbe huo kusomwa waziri mkuu alitabasamu bila kutoa jibu lolote kuhusiana na suala hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana wadau wa michezo mkoani Dodoma walisema wanatumaini uwepo wa makao makuu utaleta msukumo mkubwa katika michezo na kufanya Dodoma kuwa na timu katika ligi kuu.

ZeroDegree.
Wadau wa soka walilia uwanja wa kisasa Dodoma. Wadau wa soka walilia uwanja wa kisasa Dodoma. Reviewed by Zero Degree on 7/30/2016 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.