Loading...

Arusha Vinara wa wizi wa Umeme.

Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), limefanya ukaguzi wa miundombinu yake, kwa wateja 3,523 ambapo kati ya hao 165 walibainika kuibia shirika na kusababishia hasara ya zaidi ya bilioni 1.


Akizungumza jana katika kijiji cha Seela Sing’isi, Wilayani Arumeru wakati wa ukaguzi wa miundombinu hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa miundombinu Taifa, John Manyama, alisema ukaguzi huo wamefanya katika kipindi cha miezi tisa na kufanikiwa kupita mikoa 13 nchini.

Manyama amesema katika mikoa hiyo 13, Mkoa wa Arusha unaoongoza kwa kuwa na wezi wengi wa umeme, ukifuatiwa na mkoa wa Mwanza na Mbeya ni wa tatu, hali hii inawalazimu TANESCO wafanye ukaguzi wa mara kwa mara katika mikoa hiyo ili watu waache kuibia shirika la umma.

Amesema katika maeneo ya Mererani kwenye migodi ya madini Tanzanite, kazi yao kubwa kuiba umeme, badala ya kutumia mita wanatumia ‘cable’ ili kuiba umeme, jambo ambalo pia ni hatari sana kwao na wafanyakazi wao.

ZeroDegree.
Arusha Vinara wa wizi wa Umeme. Arusha Vinara wa wizi wa Umeme. Reviewed by Zero Degree on 8/18/2016 11:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.