Loading...

Kaya zaidi ya elfu 30 zaondolewa katika Mfuko wa Taifa wa Jamii [ Tasaf ].

Kaya 32,456 zimeondolewa katika mpango wa kuzinusuru na umasikini unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Jamii (Tasaf) kwa kukosa sifa.




Akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu mpango huo kwa wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za Kanda ya Ziwa jijini Mwanza juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga amesema wameziondoa kaya hizo baada ya kuhakiki upya.

Mwamanga amesema awali zilitambuliwa kaya milioni 1.3 lakini ziliandikishwa ni milioni 1.1, zenye sifa zikiwa na watu 6.5 milioni kutoka Tanzania bara na visiwani huku asilimia 54 wakiwa ni wanawake.


Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Kaya zaidi ya elfu 30 zaondolewa katika Mfuko wa Taifa wa Jamii [ Tasaf ]. Kaya zaidi ya elfu 30 zaondolewa katika Mfuko wa Taifa wa Jamii [ Tasaf ]. Reviewed by Zero Degree on 8/18/2016 11:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.