Loading...

Baada ya sare na JKT Ruvu, mkameroon Simba abadilisha mfumo.

MATOKEO ya sare ya bila kufungana na timu ya JKT Ruvu, yamemlazimu kocha wa Simba, Joseph Omog kubali mfumo wa uchezaji na kusisitiza umakini kwa wachezaji wake katika mechi za ligi zinazofuata.

Simba ilicheza vizuri na kuutawala mchezo huo uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya JKT Ruvu, lakini ilishindwa kupata bao kitu ambacho kimemsononesha Mcameroon huyo aliyewahi kuifundisha Azam misimu miwili iliyopita.

Akizungumza na gazeti hili jana, Omog alisema analazimika kubadili mfumo wa uchezaji kwa kucheza kwa malengo huku wakitafuta njia za kufunga mabao katika wakati mgumu kama ilivyokuwa kwenye mchezo wao na JKT Ruvu.

“Tulicheza vizuri lakini hatukupata ushindi siyo matokeo mabaya, lakini pia siyo mazuri kwa sababu ligi ina ushindani unapopata matokeo tofauti na ushindi inakuwa mbaya na sasa nimeona tubadili mfumo wa uchezaji wetu tuache kupiga pasi nyingi na sasa tunatakiwa kwenda mbele kutafuta ushindi na kila mchezaji wangu nataka aongeze umakini awapo uwanjani,” alisema Omog.

Kocha huyo alisema pamoja na kwamba matokeo ya sare siyo mabaya, lakini kama kocha hayajamfurahisha na ndiyo maana amepanga kubadili mfumo wa uchezaji kwa kutaka wacheze kwa kasi hasa wanapovuka mstari wa kati na pia atawabadili baadhi ya wachezaji ambao watashindwa kuendana na mfumo huo.

Alisema hana tatizo na uwezo waliokuwa nao wachezaji wake kwani amehusika kwa asilimia kubwa kuwasajili, bali kitu cha msingi anachokiangalia ni uwajibikaji wawapo uwanjani na kufuata kikamilifu kile ambacho amekifudhisha na baada ya dakika 90 timu ipate matokeo ya ushindi.

Kocha Omog amewataka mashabiki wao watulie na kuondoa hofu kwa sare hiyo ya Jumamosi kwani ligi ndiyo kwanza imeanza na kuna safari ndefu hadi kufikia mwisho wa kumpata bingwa wa nchi na anaimani Simba ndiyo itakuwa bingwa wa msimu huu.


ZeroDegree.
Baada ya sare na JKT Ruvu, mkameroon Simba abadilisha mfumo. Baada ya sare na JKT Ruvu, mkameroon Simba abadilisha mfumo. Reviewed by Zero Degree on 8/30/2016 03:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.