Loading...

Changamoto 5 kwa Kocha Zinedine Zidane kuelekea UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla.

Real Madrid watacheza dhidi ya Sevilla katika mchezo wa 3 mfululizo wa UEFA Super Cup ambao utahusisha timu timu za Hispania pekee, mnamo tarehe 9 August pale Trondheim Norway.

Mnamo 18 May, ushindi wa Sevilla mbele ya Liverpool jijini Basel uliwapa nafasi ya tano ya kushiriki kwenye Super Cup – mara zote wakiwa mabingwa watetezi wa UEFA Cup/UEFA Europa League. 

Siku 10 baadae, Real Madrid wakawafunga mahasimu Atlético Madrid kwa penati na sasa wanaelekea Norway kwenye Super Cup wakiwa na matumaini ya kurudia ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Sevilla mnamo 2014 katika UEFA Super Cup jijini Cardiff. Lakini siku 5 kabla ya mchezo huo, Real Madrid wana changamoto tano zinazompasua kichwa kocha wao Zinedine Zidane….

1. Kukosekana kwa mshambuliaji wa uhakika.


Magoli matatu aliyonayo Marcelo yanamfanya awe mfungaji bora wa Madrid katika michezo ya pre season inayoendelea, lakini jambo hili linatia shaka ukizingatia majeruhi ya Benzema wakati Morata bado hajafiti vizuri kwenye timu.

Zidane atakuwa bila mshambuliaji yoyote kutoka kwenye kundi la BBC katika mchezo wa fainali vs Sevilla na tayari amegundua Morata bado hajafiti kwenye mfumo wa timu. Mchezaji wa kikosi cha Castilla, Mariano anaweza kutumika baada ya kucheza vyema na kufunga katika mchezo vs Chelsea.

2. Wachezaji wasiojua hatma yao kikosini:

Suala la kudili na wachezaji wakati dirisha la usajili likiwa bado wazi, ni jambo linaloletaga shida mara kadhaa kwa kocha yoyote na Zidane ameshaongea hadharani kwamba Jese aangalie timu nyingine huku kukiripotiwa tayari kwa uwepo wa mazungumzo baina ya PSG na Madrid. 

Isco, James na Kovacic ni wachezaji wengine wa Madrid ambao hatma zao hazieleweki na klabu inaonekana ipo tayari kuwauza ikiwa watapata ofa nzuri.

3. Kutokuwepo kwa Kroos na Modric:

Huku wakiwa na pengo la Kroos na Modric katika safu ya kiungo, Isco na Kovacic walionyesha kiwango kibovu katika michezo ya kirafiki, lakini hili haliwezi kusemwa kwa Marco Asesnio, kijana wa miaka 20, amekuwa mmoja wa wachezaji bora wa Madrid katika pre season. 

Kabla ya ziara ya pre season, hatma yake ndani ya klabu ilikuwa haieleweki lakini kuelekea mchezo wa Super Cup, kinda huyu aliyezaliwa eneo la Mallorca amemshawishi Zidane na huenda akaanza, lakini bado kukosekana kwa Modric na Kroos ni changamoto nyingine inayomuumiza kichwa Zizzou.

4. Muda mfupi wa kuandaa mfumo wa 442:


Mara tu ilipo fahamika kwamba Cristiano Ronaldo hatocheza mchezo wa Super Cup jijini Trondheim, Zidane alianza kufanya maandalizi ya kutumia mfumo wa 4-4-2 kwa matumaini ya kuwatumia Morata na Benzema kwenye ushambuliaji. Majeruhi ya Benzema yamempa changamoto Zizzou ya upangaji wa kikosi huku kukiwa hakuna member hata mmoja wa BBC katika mchezo huo.

5. Maandalizi yasiyotosheleza ya Pre Season:



Real Madrid watakuwa wamecheza mechi 3 tu mpaka kufikia mchezo wao vs Sevilla, hivyo bado damu zao zitakuwa hazijakaa sawa na hili lilionekana wazi katika mchezo dhidi ya PSG ambao ndani ya dakika 30 za mwanzo, Madrid alikuwa kashapigwa 3 kwa makosa ya wachezaji ambao walionekana miili yao haikuwa na utayari. Backline ya Marcelo-Varane-Nacho-Carvajal haikuonekana pia kuwa vyema katika mchezo vs Chelsea.

Credits: ShaffihDauda
ZeroDegree.
Changamoto 5 kwa Kocha Zinedine Zidane kuelekea UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla. Changamoto 5 kwa Kocha Zinedine Zidane kuelekea UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla. Reviewed by Zero Degree on 8/05/2016 10:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.