Loading...

Haya hapa mambo manne yaliyoafikiwa kwenye mkutano wa dharura wa klabu ya Yanga.


KUFUATIA sakata la Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, kudaiwa kujiuzulu, sakata hilo limechukua sura mpya ambapo baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wametaka mwanachama mwenzao mkongwe, mzee Akilimali asimamishwe ama afutwe kabisa uanachama.



Kauli hiyo imetolewa leo kwa pamoja na viongozi mbalimbali wa matawi ya Klabu ya Yanga ambao walifanya mkutano wa dharura kwenye makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam ili kujadili undani wa sakata hilo huku wengi wao wakionekana kuwa na hasira na kuzungumza kwa hisia wakidai kuwa Akilimali ndiye anayewachanganya na anatakiwa kusimamishwa au kufutwa kabisa uanachama.

Wakizungumza mbele ya waaandishi wa habari, wanachama na wapenzi wa Yanga waliokuwa wamemiminika kwenye mkutano huo, walidai kuwa kauli tata za mzee huyo zimechangia kwa kiasi kikubwa kwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji, kuamua kujiuzulu nafasi yake kama ambavyo imekuwa ikidaiwa tangu jana.


Lawama nyingi zinaonekana kutupwa kwa mzee huyo ambaye mapema leo aliomba radhi kwa kauli zake tata, hata hivyo hakuwepo klabuni hapo wakati matamko hayo ya wanachama yakitolewa.

Mbali na viongozi kadhaa wa matawi, mashabiki wengi walionekana wakizunguka eneo la klabuni hapo kutaka kujua nini kinachoendelea na kama ni kweli Manji kaamua kujiuzulu au la, lakini hakukuwa na tamko la ziada tofauti na kile kilichoandikwa na mtandao huu kuwa Manji bado hajatoa tamko rasmi.

Mmoja kati ya viongozi wa matawi ya Yanga mkoa wa Dar es Salaam anayeiwakilisha Kanda ya Temeke, Robert Liungu, ametaja maazimio waliyofikia kutoka katika mkutano huo wa dharura.

Kwanza kabisa, wanachama wa Yanga wanatambua kuwa Manji bado ni Mwenyekiti wao kwa mujibu wa katiba yao.

Pili, wanachama wamemuomba mdhamini mzee Katunda amtoe Akilimali katika nafasi ya katibu wa wazee wa Yanga kwani ndiye anayedaiwa kumpinga Manji.

Tatu, wanachama wanaiomba Kamati ya Utendaji ya Yanga imuite Akilimali imuhoji na kumsimamisha uanachama kwa madai kuwa yeye ni Simba.

Nne, wanachama wa matawi yote wanaendelea kumtambua Yusuph Manji kama Mwenyekiti wao, alizungumza Robert Liungu.


Credits: Global Publishers
ZeroDegree.
Haya hapa mambo manne yaliyoafikiwa kwenye mkutano wa dharura wa klabu ya Yanga. Haya hapa mambo manne yaliyoafikiwa kwenye mkutano wa dharura wa klabu ya Yanga. Reviewed by Zero Degree on 8/16/2016 05:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.