Henry aitabiria makubwa timu ya taifa ya Ubelgiji.
KOCHA mpya msaidizi wa timu ya Taifa ya Ubelgiji, Thierry Henry, amesema kwamba anaamini kikosi chake kitaweka historia katika medani ya soka.
Nyota huyo wa zamani wa timu ya Arsenal, alichaguliwa wiki iliyopita ili aweze kumsaidia kocha Roberto Martinez katika jukumu la kukinoa kikosi hicho.
Kwa uteuzi huo sasa, Henry atakuwa akifanya kazi na wachezaji kama Eden Hazard, Kevin de Bruyne na Romelu Lukaku, ili kuhakikisha Ubelgiji inafanya vizuri baada ya kushindwa kuvuka hatua ya robo fainali katika michuano ya Mataifa ya Ulaya, Euro 2016, ikiwa chini ya kocha wake wa zamani, Marc Wilmots.
“Ni changamoto kubwa mno, lakini tunachokwenda kukifanya ni kujenga timu kisaikolojia ili iweze kuwa tishio,” Henry aliiambia Sky Sports.
“Mimi ni kocha msaidizi, lakini Roberto ni kocha mzuri nitamsaidia kutengeneza mipango ambayo tutahakikisha timu inafika mbali,” aliongeza kocha huyo.
Alisema anavyodhani timu hiyo itaweka historia.
Ubelgiji itaivaa Hispania Alhamisi wiki hii katika mechi ya kitaifa ya kirafiki kabla ya kuanza kampeni za kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Cyprus siku tano baadaye.

Credits: Bingwa
ZeroDegree.
Henry aitabiria makubwa timu ya taifa ya Ubelgiji.
Reviewed by Zero Degree
on
8/30/2016 02:41:00 PM
Rating: