Loading...

Hillary Cliton anashutumiwa kwa mauaji yaliyotokea Libya mwaka 2012.

Mapema mwaka huu Clinton alisafishwa kutohusika na mauaji hayo

Wazazi wa wamarekani wawili waliouliwa miaka minne iliyopita nchini Libya wanamshutumu mgombea Urais kupitia chama cha Democratic Hillary Cliton, kwa kuchangia kutokea kwa mauaji hayo.


Clinton waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani kipindi ubalozi wa Marekani nchini Libya uliposhambuliwa.

Patricia Smith na Charles Woods, ambao ni wazazi wa Sean Smith na Tyrone Wood wamesema kuwa matumizi ya barua pepe binafsi zilichangia mauaji ya watoto wao.
Patricia Smith, mama wa Sean Smith amemlaumu Clinton kwa kifo cha mtoto wake.

Msemaji wa kampeni za Hilary Clinton amepinga tuhuma hizo. Ingawa kamati ya Chama cha Republican inaweka wazi mabaya aliyoyatenda Hilary, jambo linalo tia doa kampeni zake za Urais.

Uvamizi wa majeshi ya kiislam katika ubalozi wa Marekani uliwauwa raia wanne wa nchi hiyo akiwemo Balozi Chris Stevens.


Credits: BBC
ZeroDegree.
Hillary Cliton anashutumiwa kwa mauaji yaliyotokea Libya mwaka 2012. Hillary Cliton anashutumiwa kwa mauaji yaliyotokea Libya mwaka 2012. Reviewed by Zero Degree on 8/10/2016 08:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.