Japan yaahidi msaada wa dola bilioni 30 barani Afrika.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akihutubu wakati wa ufunguzi wa kongamano la maendeleo barani Afrika, Kenya, 27 Agosti 2016. |
Theluthi ya pesa hizo itatumika kufadhili miradi ya miundo mbinu.
Bwana Abe ametoa ahadi hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la maendeleo barani Afrika nchini Kenya.
Kwa mara ya kwanza kongamano la sita la kimataifa la Tokyo kuhusu maendeleo barani Afrika (TICAD-VI) limeandaliwa barani Afrika.
Kongamano hilo limevutia wajumbe 10,000 na marais zaidi ya thelathini kutoka nchi za afrika, ambapo Japan inajaribu kurejesha ushawishi wake wa awali, na masoko ya nje, ambayo yamenyakuliwa na Uchina.
Wawakilishi wa mataifa ya bara la Afrika katika kongamano la sita la Tokyo la maendeleo barani Afrika, Nairobi, nchini Kenya.
Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
|
Japan yaahidi msaada wa dola bilioni 30 barani Afrika.
Reviewed by Zero Degree
on
8/28/2016 10:13:00 AM
Rating: