Loading...

Kikosi cha kwanza Simba pasua kichwa.

Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja
KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kazi kubwa wanayokumbana nayo katika kikosi chao cha sasa ni kupata timu ya kwanza.

Akizungumza baada ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA ya Uganda mwishoni mwa wiki iliyopita, Mayanja alisema kila mchezaji wa timu hiyo ni mzuri na hivyo benchi la ufundi linachanganyikiwa namna ya kupanga kikosi.

“Simba ya mwaka huu ni bora kutokana na aina ya wachezaji tulionao maana wanaoanza kikosi cha kwanza na wanaokaa benchi wote wakali, hivyo kazi ya kocha Joseph Omog na benchi la ufundi inakuwa ngumu,” alisema.

Alisema jambo kubwa kwa sasa ni mashabiki kuendelea kuiamini na kuiunga mkono timu yao ili itemize lengo la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

Matokeo ya mechi hiyo na URA yalikuwa sare ya bao 1-1.

Aidha Simba ilitumia mechi hiyo kumuaga nahodha wake wa zamani, Mussa Hassan Mgosi aliyestaafu rasmi na kuwa meneja wa timu.

Mayanja alisifu uongozi wa Simba kwa jambo hilo na kusema inatia hamasa kwa wachezaji wengine kuona mwezao aliyeitumikia klabu miaka mingi akipewa nafasi ya kuwa meneja.

“Mgosi ameitumikia vizuri Simba kwa kipindi chote alichocheza na namtakia kila lenye heri katika maisha yake mapya nje ya uwanja”. Mbali na Simba, Mgosi pia amecheza JKT Ruvu, Mtibwa Sugar na Motema Pembe ya Congo DR.


Credits: Habari Leo
ZeroDegree
Kikosi cha kwanza Simba pasua kichwa. Kikosi cha kwanza Simba pasua kichwa. Reviewed by Zero Degree on 8/16/2016 09:23:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.