Madai ya uchawi yasababisha vifo vya wazee 14 Kahama.
wazee wanashitumiwa kuwa wanashiriki uchawi. |
Kati yao 14 waliuawa kwa kuhusishwa na tuhuma za uchawi na imani za kishirikina ambao wengi ni wazee, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Murilo Jumanne, alisema.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, alisema kuwa kiwango hicho ni kikubwa mno hakiwezi kufumbiwa macho na Jeshi la Polisi.
“Kwa Januari idadi ya watu waliouawa ni wawili, Februari watatu, Machi watano, Aprili waliuawa watu wanne, Mei watu wanne na Juni walikufa watu watatu,” alisema na kuongeza: “Wastani wa mtu mmoja hufariki dunia kila wiki kwa ajali za barabarani katika wilaya hii hivyo kuna haja ya watumiaji wa vyombo vya usafiri kupewa elimu ya usalama barabarani.”
Kufuatia hali hiyo, Kamanda aliwataka madiwani na viongozi wa serikali za mitaa na vijiji kuendelea kutoa elimu ili watu wasijihusishe ama kushiriki katika mauaji ya wazee na wahamasishwe kuhusu umuhimu wa kutoa ushahidi mahakamani pale mhalifu anapofikishwa kortini ili kuwatia hatiani wauaji hao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, aliwaomba madiwani na viongozi wengine kuona umuhimu wa kushirikiana na polisi, pamoja na serikali kutokomeza mauji ya wazee ambayo yanaendelea katika Wilaya ya Kahama.
Alisema Wilaya ya Kahama inaongoza kwa vitendo vingi vya uhalifu na kuinyima usingizi Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
ZeroDegree.
Madai ya uchawi yasababisha vifo vya wazee 14 Kahama.
Reviewed by Zero Degree
on
8/14/2016 04:22:00 PM
Rating: