Majaliwa agoma kupokea madawati yaliyochini ya kiwango.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati, uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango.
Waziri Mkuu aligomea madawati hayo jana wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi, ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS.
Alisema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati, lakini hawezi kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.
"Ofisa Elimu njoo, kagua haya madawati, yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya, huu si wakati wa kupokea vitu vibovu," alisema.
Baada ya Ofisa Elimu (Msingi) wa Wilaya ya Mvomero, Michael Ligola kukagua madawati 102 yaliyoletwa uwanjani hapo, madawati 84 yalibainika kuwa ni mabovu na 14 tu ndiyo yalikuwa mazima.
Waziri Mkuu alisema hawezi kupokea madawati hayo yaliyotolewa na Meneja wa Msitu wa Mtibwa, Hamza Kateti na kuuagiza uongozi wa wilaya, ufuatilie suala hilo kwa kuwa walitakiwa kuyakagua, kabla ya yeye kukabidhiwa.
Katika hatua nyingine, aliwasisitiza wazazi na walezi wa wilaya hiyo, kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Serikali imewapunguzia mzigo kwa kuwaondolea michango na ada, hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuwapeleka shule watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule na wasimamie masomo yao," alisema.
Awali, Mbunge wa Mvomero, Suleiman Saddiq ‘Murad’ alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili wilaya hiyo ni pamoja na wafugaji kuingiza mifugo katika mashamba, hivyo alimuomba Waziri Mkuu kuingilia kati suala hilo.
Akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima, Waziri Mkuu alisema wafugaji wenye mifugo mingi, watahamishiwa katika vitalu vinavyomilikiwa na ranchi za Taifa ; na wenye mifugo michache watatengewa maeneo katika vijiji.

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Majaliwa agoma kupokea madawati yaliyochini ya kiwango.
Reviewed by Zero Degree
on
8/03/2016 09:22:00 AM
Rating: