Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [ NIDA ] kutoa namba kwa waliojisajili NEC.
NIDA iko mbioni kuanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi waliosajiliwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumza kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ya Ngongo, Lindi, Afisa uhusiano wa NIDA, Rose Mdami alisema ifikapo Desemba 31 mwaka huu, watanzania wote watakuwa na namba za utambulisho ambazo watazitumia kama vile kitambulisho cha taifa.
“Wananchi waliosajiliwa kwenye Daftari la Wapigakura la NEC ambao hawajapata na kusajiliwa kwa ajili ya vitambulisho vya taifa watapewa namba ya utambulisho na kuanza kufaidi utambulisho wao kwa kupata baadhi ya huduma wakati wakiendelea na taratibu nyingine za kukamilisha usajili ili kupata usajili kamili.
Aliongeza,“wakati wanasajiliwa NEC walijaza vipengele 34, wakati kitambulisho cha Taifa kinamtaka mtu kujaza vipengele 72, hivyo wananchi ambao watapewa namba za utambulisho ili usajili wao ukamilike watatakiwa kukamilisha maswali yaliyobaki.”
Alisema hatua hiyo ni kutokana na kuchukua kanzi data ya NEC ambayo wataitumia katika kuwapa namba ya utambulisho ya taifa. Akizungumzia ushiriki wa NIDA kwenye maonesho ya Nanenane, Mdami alisema taasisi yake ina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alisema kwa kupitia mfumo huo wakulima, wafugaji na wavuvi watapata huduma kirahisi na kutambulika kirahisi.
”Kupitia mfumo wa NIDA utoaji wa ruzuku za pembejeo za kilimo, zana na uvuvi na wafugaji unakuwa ni rahisi na kuwafikia walengwa. Pia utarahisisha utoaji fidia za majanga katika shughuli za kilimo, uvuvi na mifugo.”

ZeroDegree.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [ NIDA ] kutoa namba kwa waliojisajili NEC.
Reviewed by Zero Degree
on
8/07/2016 09:01:00 AM
Rating: